Jumatatu , 20th Jun , 2016

Msanii ambaye ni rapper wa kike kutoka hapa Bongo, Stosh, amesema kuwa alipata wakati mgumu wakati anaanza game, kwani alikuwa na hofu jinsi ya muonekano wake ulivyo.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Stosh amesema alianza muziki muda mrefu sana kabla hajaanza kurap, kwa kuandika mistari na kuwapa wasanii wengine waimbe, ambao nao walikuwa kwenye harakati za kutoka kimuziki.

Stosh aliendelea kusema kuwa aliamua kuwapa watu wengine kuimba badala ya yeye mweyewe, akihofia jinsi muonekano wake wa kike ulivyo, na jinsi aina ya muziki huo ulivyo.

“Nilikuwa naandika nawapa watu wanaoenda kwenye haya mashindano ya kuimba, naandika nawapa wanarap wao, sasa kuna siku nimeandika nikampa mtu, nikawa nampeleka mahali kuimba, yule niliyemwendea akasema mbona wewe una uwezo mkubwa tu kuliko hawa unaoniletea? Nilikuwa nina hofu jinsi nilivyo, nikiangalia na aina ya muziki nikawa nahofia', alisema Stosh.

Pia Stosh ambaye ameachia wimbo wake mpya akimshirikisha Ayler, amesema kuwa muziki wa sasa una changamoto tofauti na ule wa zamani, kwani muziki wa sasa unahitaji pesa kuwekeza, tofauti na muziki wa zamani ambapo watu wengi walikuwa wanaangalia kipaji cha mtu, na kumuwezesha kutoboa.

“Kipindi cha kina Witness ilikuwa msanii anaangaliwa talent kupata sapoti, sasa hivi muziki umekuwa ni business, kwa hiyo lazima u-invest ndio utoke, lakini kama watakuwepo watu watakaojitokeza kupush watakuwepo female rappers wengi tu”, alisema Stosh.