
Msanii Gakuba Didier marufu kwa jina la Muchoma anayetokea nchini Rwanda ameachia ngoma yake mpya inayojulikana kwa jina la 'My love' ambapo anajaribu kueleza alivyompenda binti.
Muchoma ambaye kwa sasa makazi yake ni huko USA Austin Texas anasema wimbo huu wa 'My love' ni wimbo unaohusu mapenzi ambapo anakuwa amempenda binti lakini wazazi wake hawamtaki.
"Wimbo wangu huu mpya wa 'My love' unazungumzia mapenzi ya watu wanaopendana ila matatizo yanatokea katika mapenzi yao kwa kuibuka vitu tofauti tofauti, ndio maana ukitazama video utagundua kuwa wawili hao walipendana lakini tatizo likaja kwa wazazi kuwa hawataki kijana wao amuoe demu mzungu". Alisema Muchoma
Msanii Muchoma huko nyuma amewahi kuachia album ya ngoma 11 kama vile Asante , holla , coco remix , Sarah ambazo ni ngoma zilizomtambulisha sana kwenye gemu na watu wakamfahamu.
"Malengo Yangu ni kuwa hivi karibuni nafikiria kuhamia Tanzania ili nije nifanye muziki nikiwa hapo kwasababu Tanzania imekua big industry hadi Afrika nzima imeshajua hivo" Amesema Muchoma
Pia kwa sasa Muchoma amesema anafikiria kufanya collabo na wasani wengi lakini bado hajajua kabisa aanze na nani.
Bofya hapa kutazama wimbo huo wa 'My love' https://www.youtube.com/watch?v=AaUfedeFZGg