
Shaa ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Television, na kusema kwamba ingawa tatizo hilo lilikuwepo toka zamani, lakini watu walikuwa hawalizungumzii tofauti na sasa.
“Hili tatizo lilikuwepo lakini tulikuwa hatuzungumzii, sasa hivi imefika point mtu ana admit mimi nilikuwa mtumiaji, sasa the fact kwamba wanasema na kuhamasisha watu kuacha kutumia, ni hatua nzuri”, alisema Shaa.
Shaa ameendelea kueleza kwamba yeye kama msanii kazi yake kubwa ni kuelimisha jamii kupitia sanaa yake, na si kuandamana kupinga vitendo hivyo.
“Mimi kama msanii nitahamasisha tu kupitia kazi yangu ya muziki, jukumu langu ni kwenye muziki, siwezi sema niandamane mpaka labda wizarani sijui kupiga vita, nitahamasisha kupitia muziki wangu”, alisema Shaa.
Pamoja na hayo ameongelea wimbo wake mpya wa Toba ambao unaendelea kufanya vizuri kwenye vituo vya runinga vya ndani na nje, na kukiri kuwa wimbo huo amendikiwa na kuwataka wasanii wawe wawazi pale inapotokea ameandikiwa wimbo, kwani pia wanakuwa wanatoa fursa kwa wengine na kubadilisha ladha ya muziki.
“Wimbo wa toba nimeandikiwa kweli, umeandikwa na H Mbizo, unajua ni kitu cha kawaida kwa msanii kuandikiwa lakini wengi wanaogopa kusema ukweli, hata hao wasanii wa nje wanaandikiwa, Chriss Brown anaandikiwa, Beyonce anaandikiwa, Celin Dion anaandikiwa sembuse mimi Shaa”, alisema Shaa.