Jumanne , 1st Nov , 2022

Staa wa mziki Africa Davido na mpenzi wake Chioma wamempoteza mtoto wao wa kiume mwenye miaka mitatu Ifeanyi baada ya kufariki dunia ndani ya 'Swimming pool' ya familia huko Lagos Nigeria.

Picha ya pamoja ya Davido, Chioma na mtoto wao

Taarifa ya chanzo cha kifo chake kinaeleza kuwa mtoto huyo alizama chini ya maji kwa muda mrefu kabla ya kuonekana pia walijaribu kumkimbiza Hospitali ambapo ndio ilithibitishwa kwamba tayari amefariki.

Ifeanyi amefariki ikiwa imepita siku 10 tu tangu alivyotimiza miaka mitatu.