Jumatatu , 20th Oct , 2014

Msanii wa muziki Peter Msechu ambaye muonekano wake umekuwa ukibadilika na staa huyu kuonekana kuwa ameridhika sana na maisha na kunenepa, amesema kuwa unene wake ni asili kutoka katika familia yao na amekuwa akifanya jitihada kubwa kujiweka fiti.

Peter MSechu

Msechu amesema kuwa alipokuwa mdogo mwili wake ulikuwa umetuna kiasi cha mtu kutokuweza kutambua jinsia yake akiwa amevaa mavazi ya tofauti, na kwa mashabiki wake ambao wamekuwa na mtazamo tofauti juu ya muonekano wa mwili wake, hivi ndivyo anavyowachana.