Ijumaa , 4th Sep , 2015

Star wa muziki wa nchini Uganda, Moze Radio ameripotiwa kurejea katika tabia yake ya awali ya kupiga mtungi kupindukia, hii ikiwa ni baada ya kutangaza kuachana na vilevi ikiwepo uvutaji wa bangi siku 16 zilizopita.

Moze Radio

Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na star huyo, Radio alianza vizuri mpango huo, tangu kupata msukumo wa wanafamilia na rafiki wa karibu na baada ya muda alishindwa kujizuia na kuanza kunywa tena kwa kujificha mpaka sasa ambapo tabia yake hiyo imerejea kwa kasi kubwa.

Hata hivyo kwa mujibu wa wafuatiliaji wa mambo tabia ya unywaji na uvutaji ya msanii huyo kwa sasa imeelezwa kuchochewa na msongo wa mawazo unaochangiwa na mahusiano yake na msanii Lilian Mbabazi ambayo hayaendi vizuri.

Tags: