Jumanne , 6th Oct , 2015

Mshindi wa shindano la Big Brother Africa, Hotshots Idris Sultan amesema haoni shida kutumia muda wake mwingi katika mitandao ya kijamii kwa kuwa kwake ni sehemu mojawapo ya kazi.

Idris ambaye hivi karibuni amekua akijulikana zaidi kama mchekeshaji (comedian) ametamka hayo kwenye mahojiano katika kipindi cha Mkasi kinachorushwa na kituo cha EATV.

“Ukiwa mtu maarufu watu wanahitaji kukuona muda wote na huwezi kupata interview (mhojiano) kila siku hivyo sehemu pekee unapoweza kuwa karibu na watu ni kwenye mitandao ya kijamii, kwa hiyo mimi naichukulia kama kazi yangu pia,” alisema na kuongeza mchekeshaji huyo.

Kauli hii ya Idris inafuatia swali aliloulizwa na mtangazaji machachari wa kipindi hicho Salama Jabir aliyemtaka kujibu tuhuma kutoka kwa mashabiki wanaodai hana kazi maalum kutokana na muda mwingi anakua kwenye mitandao ya kijamii.

Aidha, Idris amekanusha madai yaliyowahi kutolewa hapo awali kuhusu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji filamu Wema Sepetu. Akizungumzia uchekeshaji amefunguka na kusema ni moja ya vitu anavyopenda kufanya na anajitazama katika soko la kimataifa la uchekeshaji huku akimtaja Kelvinn Hart kama sehemu ya watu anaowaza kushirikiana nao siku