Jumatatu , 14th Sep , 2015

Staa wa miondoko ya bongofleva Bwana Misosi amesema kuwa huu mwaka umekuwa wa kihistoria kutokana na kile ambacho vyama pinzani vinataka kuonesha mabadiliko kuelekea kampeni za wagombea katika nafasi mbalimbali za urais na uongozi nchini.

Staa wa miondoko ya Bongofleva Bwana Misosi

Mkali huyo aliyetamba na kibao cha 'Nitoke Vipi' amesema kwa muda huu ambao vuguvugu la uchaguzi mkuu likiendelea nchini, ni wakati mzuri wa kujiandaa na kutoa kazi mpya ikiwemo pia kufanya maandalizi ya kufanya Listening Party ya ngoma hiyo mpya.