Jumatano , 22nd Apr , 2015

Msanii Michael Ross wa Uganda ameripotiwa kujichimbia mafichoni baada ya tukio la mwishoni mwa wiki la kufukuzwa katika nyumba aliyokuwa akiishi huko Makindye kutokana na malimbikizo ya deni la kodi katika kipindi cha miezi 6 mfululizo.

msanii wa muziki nchini Uganda Michael Ross

Kwa mujibu wa chanzo cha taarifa, msanii huyo amekuwa akimuongopea mdeni wake kuwa yupo nje ya nchi kikazi, wakati ikiwa inafahamika kuwa makazi yake kwa sasa amehamishia kwa mpenzi wake Aline Kemigisha.

Michael Ross mpaka sasa hajapatikana kueleza upande wake wa habari hizo kutokana na kuonekana kwake kuwa ni kitu adimu sana.