Ijumaa , 17th Oct , 2014

Msanii na mtayarishaji muziki Mensen Selekta, ameweka wazi kuwepo kwa kazi kadhaa za kimataifa katika studio yake ya Defatality zikiwa ni mkakati wa kujitangaza kimataifa pale zitakapotoka.

Mesen Selekta

Mensen Selekta amesema kuwa, yeye pamoja na timu yake akishirikiana kwa karibu na rapa Viva Consious, tayari wameshafanikisha kufanya rekodi na baadhi ya wasanii kutoka Marekani, Ghana na sehemu nyingine.