MAYUNGA
Mayunga amefunguka na kutufahamisha kuwa ana mashabiki wengi sana nje ya bongo na hilo amelitambua alipokuwa ameenda nchini Nigeria kutambulisha nyimbo zake na kuona kuwa anakubalika nchi mbalimbali.
Pia Mayunga ameiambia Enews kuwa anaendelea kujipanga ili azidi kutoka kimatafa zaidi na kuendelea kutambulisha nchi yake katika nchi mbalimbali kwa kuwa anaamini mziki wa Tanzania ni mzuri ila unahitaji tu uzalendo kwa wingi.
Mayunga amesema pia ana mipango ya kufanya kazi na king wa RnB Ben Pol huku akisema ni msani wa bongo ambaye anamkubali sana huku akisema ni moja kati ya wasanii wanaofanya vizuri sana hapa Tanzania.








