Ijumaa , 30th Mei , 2014

Maurice Kirya, Staa wa muziki wa nchini Uganda amesema kuwa, tetesi ambazo zinaendelea kusambaa mtandaoni kwa sasa kuhusiana na yeye kuwa na mahusiano na mrembo Flavia Tumusiime, hazina ukweli wowote.

Maurice ameweka wazi kuwa, ana wasiwasi juu ya madhara ambayo tetesi hizi zinaweza kusababisha kwa upande wa Flavia, kutokana na tetesi hizi kuongezewa nguvu kwa namna ambavyo wawili hawa wameonekana kuelewana kwa namna ya pekee wakiwa karibu.

Hii si mara ya kwanza kwa Maurice kukabiliwa na tetesi kuhusiana na mahusiano yake kutokana na kutokuwa muwazi katika swala hili, ambapo itakumbukwa kuwa alikwishawahi kuhusishwa na mahusiano na msanii na mwanamitindo Brenda Nambi.