Staa wa muziki wa kike nchini Maua Sama
Mkali huyo ameeleza kuwa, hii inakuwa ni nafasi nzuri kama msani kuendelea kuongeza rekodi ambapo hapo baadaye atakuwa na wigo mkubwa wa kuchagua ni ipi bora ambayo atatoka nayo, baada ya kuisha kwa harakati za uchaguzi mkuu.
Msanii huyo pia akagusia joto la kisiasa hapa nchini kwa sasa, ambapo amesema ni dalili kuwa watanzania wanataka mabadiliko, akiwataka kuvuka hatua hiyo kwa kudumisha amani na utulivu huku tukibakia na umoja wetu.




