Jumamosi , 28th Mar , 2015

Mpambano mkali kabisa wa masumbwi, Night of Knockoutz ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee usiku wa Jana umekuwa na burudani ya aina yake kwa umati mkubwa uliohudhuria tukio hilo.

JB na Kiberenge katika mahojiano Diamond Jubilee usiku wa kuamkia leo.

Pambano hilo mwisho wa siku lilishuhudia bondia mtanzania Mohamed Matumla akimshinda kwa pointi mpinzani wake kutoka china, Bondia Wan Xin Hua.

Miongoni mwa mashabiki waliojitokeza kushuhudia mpambano huo, Mastaa mbalimbali kutoka tasnia ya Filamu na vile vile muziki wameweza kuhudhuria na kuweka wazi hisia zao juu mvuto mkubwa wa burudani ya mchezo wa masumbi, na vilevile kuishukuru EATV na EA Radio kwa udhamini wao wa nguvu kuwezesha tukio hilo kama wanavyonukuliwa hapa.

BABU TALE; "Mimi ngumi ndio burudani yangu, si unajua mi natokea uswahilini bana, na boxing ndiyo michezo yetu, nimefurahishwa sana na tukio la mipambano ya leo, japo nilichelewa kidogo kufika lakini nime-enjoy sana, Big ups kwa East Africa Radio na East Africa Television".

SHETTA; "Mimi binafsi sijawahi kuhudhuria mapambano ya ngumi, lakini leo hii nafikiri ndio itakuwa muendelezo wa kuhudhuria mapambano kama haya, kiukweli nimefurahi sana, sijawahi kuamini kama kuna mtu anaweza akapigwa hadi akalala chini na kushindwa kuendelea tena, ila leo nimejionea mwenyewe, Big Ups EATV na East Africa Radio.

TUNDA MAN; "Kiukweli, sijutii muda wangu kuwa hapa, East Africa Television wamejipanga, hata umati wote huu tunaouona hapa ni ishara kuwa wametangaza vizuri na kujipanga vizuri kuandaa mpambano huo, kiukweli nimefurahi sana".

KHALID CHOKORAA; "Hii ni ishara kuwa, media ikiamua kukishikilia kitu, kinafanikiwa kwa kiasi kikubwa, Boxing imekuwa chini, lakini EATV, EA Radio wameonyesha mfano na kuishikilia mpaka leo kuandaa kitu kikubwa kama hiki".

JB; "Kabla ya kufika hapa, sikudhani kama ntaburudika kama nilivyoburudika leo, asee hii sio mchezo".

Kwa taarifa zaidi kutoka tukio hilo lililohusisha mapambano 6 makali ya ngumi, usikose kutazama Muhtasari wa michezo leo hii saa 8 40 usiku, hapa EATV pekee, wenyewe wanasema ni #NgumiTu