Jumatatu , 24th Mei , 2021

Msanii Dogo Janja "Janjaro" amesema kuna muda mtu unapitia changamoto za kimahusiano mpaka unatamani ujiue au ujidhuru lakini ukifikiria kuna mama yako anakutegemea basi unaacha kufanya jambo hilo.

Msanii Dogo Janja

Dogo Janja amezungumza hilo kwenye show ya Planet Bongo ya East Africa Radio, wakati anatambulisha Album yake mpya ya Ahsante Mama aliyowashirikisha wasanii wa kike tu.

"Mama ni mtu ambaye hata ukiwa umekosea anakuwa upande wako kwanza halafu atakuonya mkiwa wenyewe na hawezi kuwa na ushauri mbaya, vijana wakipata maswaibu wanapoteza matumaini wanaingia kwenye madawa, anakuwa mlevi wa kupindukia"

"Lakini ukiwa na mtu kama mama yako unajua ukifanya vitu hivi utamuumiza itakusaidia vitu vingi kama ukimuweka mama kwenye nafasi hiyo, usiishi kama hauna cha kupoteza kuna muda unapitia mapenzi unatamani hata ujiue au ujidhuru lakina unafikira kuna mama".