Alhamisi , 13th Jan , 2022

Wasanii maarufu ambao ni mapacha Tagwayen Asali kutoka Mji wa Kano Nigeria wame-make headline baada ya kufunga ndoa siku moja na wanawake mapacha wanaoitwa Hassana na Hussaina.

Picha ya mapacha wa kiume waliowaoa mapacha wa kike

Unaambiwa mapacha hao wakiume walikuwa wana ndoto siku moja waje kuoa wanawake mapacha wanaofanana na wanamshukuru mungu kwa kujibu maombi yao.

"Kufunga ndoa na mapacha wanaofanana ni moja ya matakwa ambayo tumekuwa tukitafuta maisha yetu yote na Mungu uwe utukufu tumefanikisha hilo," amesema mmoja wa mapacha hao.

Chanzo : Instablo9ja, Daily Trust, Viral Nigeria, Ghgossip.com, Globalupfornt.