Ijumaa , 30th Oct , 2015

Mtayarishaji muziki Man Water mwenye rekodi ya kushinda tuzo za mtayarishaji muziki bora mara kadhaa hapo nyumbani ameanza kutoboa mawimbi katika anga za kimataifa ambapo amefanikiwa kupata uteuzi katika tuzo maarufu za kimataifa.

Mtayarishaji muziki wa nchini Tanzania Man Water

Man Water ameeleza kuwa, kutokana na kazi zake bora, ameweza kuonekana nje ya mipaka ya Tanzania na hapa anaeleza mwenyewe zaidi juu ya tuzo hizo ambazo amefanikiwa kuingia kuziwania.