Rapa Nikki wa Pili.
Nikki ameyasema hayo alipofanya mahojiano maalumu katika kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na kituo cha EA Radio.
''Mwezi umemalizika lakini isiwe mwisho wa watu kutenda mambo mema, ni vyema mambo mema yakaendelea ili tuweze kuwa na amani zaidi;'' amesema Nikki
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani umemalizika ambapo waislamu nchini wameungana na wenzao ulimwenguni kusherehekea sikuuu ya Eid el Firi ambapo viongozi wa dini pamoja na wanasiasa wote wamezungumza lugha moja ya amani na mshikamano wa taifa letu.
Mufti wa Tanzania Abubakari Zuberi alitumia Baraza la Eid kuwashauri watanzania kupinga kwa nguvu zote ndoa za jinsia moja zinazozidi kushika kasin katika maeneo mengi duniani na ndani ya jamii.



