
mama mzazi wa msanii wa nchini Uganda Navio, Maggie Kigozi
Kwa mujibu wa taarifa, majambazi hao waliingia katika nyumba ya mama huyo baada ya kufumua vigae na kutoboa dari ambapo baada ya kuingia walitumia kisu kumjeruhi mama huyo.
Kwa mujibu wa wana usalama, majambazi hayo yalifanya uvamizi huo majira ya saa 10 alfajiri na kutekeleza unyama huyo, zoezi la uchunguzi likiwa katika mchakato.
Hivi sasa taarifa kamili kutoka kwake Navio ameiambia eNewz kuwa tayari mama yake mzazi amepatiwa matibabu hospitalini na kuruhusiwa kurudi nyumbani kwake.
