Ijumaa , 2nd Jul , 2021

Mtayarishaji mkongwe na Godfather wa Bongo Fleva P-Funk Majani ametangaza rasmi kustaafu kufanya kazi ya utayarishaji muziki (producer) baada ya kukitumikia kiwanda hicho kwa zaidi ya miaka 28.

Picha ya Mtayarishaji P-Funk Majani

Sasa ameamua kugeukia maisha mapya ya kuandaa filamu na video za muziki huku muda mwingi akiwa amepanga kufanya safari za maeneo tofauti kufurahia mazingira.