Mahari ya Bright kwa Binti wa Nyoshi El Sadaat

Ijumaa , 16th Jul , 2021

Star Kid wa BongoFlava Bright Music ameweka wazi kwamba yupo kwenye mahusiano na binti wa msanii nguli wa muziki wa Dansi Nyoshi El Sadaat, ambapo amesema mwisho wa kutoa pesa kama mahari kwa ajili ya ndoa basi ni Milioni 5 tu.

Nyoshi El Sadaat upande wa kushoto, kulia ni Bright Music

Akifunguka hilo kupitia EATV & EA Radio Digital Bright Music Music amesema 

"Suala la ndoa bado ila kila kitu kitaenda sawa na taratibu zitafuata, kuhusu mahari siwezi kuzungumza labda Nyoshi El Sadaat mwenyewe aseme kwa sababu ni mali yake, ila mwisho wangu wa kutoa Mahari ni Tsh Milioni 5 kushuka chini".

Pia ameendelea kusema mahusiano yao yamedumu kwa muda mrefu sasa tangu wawe pamoja miaka mitatu iliyopita japo mwanzoni hakutaka kuweka wazi mapema.

Zaidi mtazame hapa chini kwenye video.