Alhamisi , 12th Nov , 2015

Msanii wa muziki wa pop duniani toka Marekani Madonna, amesema ana nidhamu sana na maisha yake hivyo hajihusishi na mitandao ya kijamii mara kwa mara.

Madonna mwenye umri wa miak 57 na watoto wanne, amesema kuwa maisha yake yanazunguka sana kazi zake na kulea watoto wake.

“Nina maisha ya nidhamu sana, sijihusishi sana na mitandao maisha yangu yanazunguka sana maonesho yangu na watoto wangu, na kujaribu kuishi maisha ya afya nzuri, kitu pekee ninachopungukiwa kwa sasa ni kulala”, alisema Madonna.

Mama huyo wa watoto Lourdes (19), Rocco 1(5) ,Mercy na David wemye miaka 9, kwa sasa yuko kwenye ziara yake ya 10 ya dunia na kukiri kuwa inakuwa ngumu kwa yeye kumudu yote hivyo analazimika kuacha baadhi ya vitu anavyopenda kuvifanya.

“Ni ngumu kuchagua, muda mwingine naacha vitu vingine ninavyovipenda kwa sababu haviendi sawa na hali iliyopo, ni lazima niwe mkatili muda mwingine, ni kama kuhariri filamu kuna vipande unavyovipenda unavikata kama havileti ujumbe kwa watu”, alisema Madonna