
Hayo yameibuka baada ya Nancy ku-post picha ya pamoja yeye na Roma katika mtandao wa kijamii wa instagram na kuandika maneno yenye kumtia faraja mume wake kwa kusema 'Be a friend encourage someone take time to care. Let your words heal and not wound'
"Apone basi na yeye asijilegeze kha! wanaume wa tanga bana" Ali-comment Madee
Akajibu Nancy...."Nimewaona marafiki na baadhi ya wasanii wakija kumuona, nilitegemea wewe ungekuwa wa kwanza kuja kumuona rafiki yako, ndugu yako, mtani wako lakini huu ni mwezi umekatika sijaona hata ukimpigia simu ! wala kuja kumjulia hali, hakika nimejifunza mengi sana kipindi hiki, ubarikiwe sana shemeji yangu Hamad, msalimie mtoto wetu Saida".
Kwa pamoja Team ya East Africa Radio na EATV tunamtakia Roma Mkatoliki apone salama..