Jumatatu , 19th Jan , 2015

Msanii AY ambaye atapanda jukwaani Jumamosi hii kutumbuiza katika tamasha la Tigo Kiboko Yao, amejitapa kuwashtua watu kwa aina ya onesho atakalofanya Jumamosi hii na kuacha mfano ambao utaigwa na wengine.

Msani wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania AY

AY amesema kuwa, licha ya kufanya maandalizi mengine ya kawaida kwa ajili ya onesho, show atakayofanya inaandaliwa katika karatasi na vilevile kompyuta, sababu ya msingi kabisa kwako kujipanga kuja kushuhudia ni nini atakachofanya pale juu ya jukwaa.