Alhamisi , 25th Jun , 2015

Star wa filamu wa kimataifa mwenye asili ya Kenya, Lupita Nyong'o anatarajia kutua nchini humo kwa ziara maalum kunyanyua jumuiya ya kisanaa na vilevile kuongeza uelewa katika jitihada za uhifadhi wa maliasili.

Lupita na Wazazi wake

Star huyo ameweka wazi tarehe 29 mwezi huu kama siku kubwa ambayo ndio atakapotua nchini humo, ambapo atapata nafasi ya kukutana na wanafunzi, wasanii na kujadiliana nao mambo mbalimbali ikiwepo mafanikio yake katika sanaa.

Hii inakuwa ni hatua kubwa kwa star huyo kuifanya, akitumia jina nafasi na uwezo wake kusaidia nchi yake kupiga hatua katika maeneo hayo muhimu kabisa kwa maendeleo ya taifa.