
Elizabeth Michael 'Lulu'
Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Mwl.J.K. Nyerere, Agosti 28 unahusu haki miliki za wasanii, mirabaha na mchakato wa wasanii kusajili katika Baraza la Sanaa Tanzania BASATA, lililopo chini ya Wizara hiyo.
Akizungumza EATV & EA Radio Digital kuhusu wasanii waliokosekana katika mkutano huo Lulu amesema, “huwezi kumsemea mtu kwa sababu gani labda hajafika, huwezi jua labda anauguliwa au alikuwa njiani akapata dharura. Kikubwa ni kwamba tuliokuwepo hapa tuwe wawakilishi wazuri, tuwe mabalozi wazuri tukafikishe hiki ambacho tumekisikia hapa”.
Aidha ameendelea kusema anaiyona mbali tasnia ya filamu kwa miaka ijayo kwa sababu hata serikali inatambua jitihada zao na wamesikia kilio cha wasanii kuiomba serikali kutoa msaada katika masuala yao mbalimbali.
Pia Lulu amesema haitakuwa rahisi kuingia katika mfumo huo wa mirabaha lakini ni bora waingie na kuona changamoto zake wakiwa ndani kuliko kutoingia kabisa.