Jumatatu , 12th Dec , 2016

Msanii nyota wa filamu nchini Tanzania Elizabeth Michael 'Lulu' ameelezea furaha yake ya kuwa msanii wa kwanza wa filamu nchini kupata nafasi ya kukabidhi tuzo katika tuzo za kwanza kubwa Afrika Mashariki za muziki na filamu, EATV Awards

Alichokiandika Lulu kuhusu EATV Awards

LuLu pia ameipongeza EATV kwa kuanzisha tuzo na kwa maandalizi yaliyofanyika katika tukio zima la utoaji wa tuzo hizo, lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Amesema anajiona wa pekee katika tasnia ya filamu Afrika Mashariki kukabidhi tuzo kwa msanii mwenzake wa kike Chuchu Hans ambaye ndiye aliyeibuka mshindi wa tuzo ya Muigizaji Bora wa kike.

Lulu aliambatana na mtangazaji wa 5Selekt TBway

Msikilize hapa Lulu akifunguka....

 

Tags: