Alhamisi , 2nd Feb , 2017

Msanii Linex Mjeda ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Kiherehere' amefunguka na kusema ule mpango wake wa kutoa wimbo mmoja kwa mwaka kwa sasa hautakuwepo tena ila mwaka huu 2017 ni ngoma baada ya ngoma.

Linex

 

Linex alisema hayo kwenye kipindi cha Friday Night Live na kusema siku ya wapendao ataachia wimbo wake mwingine mpya kama 'Bonus truck' kwa mashabiki zake ambao anasema hataufanya 'official' ila anaamini ni wimbo utakaofanya vizuri.

Mbali na hilo Linex alisema alikuwa anakaa muda mrefu bila kutoa ngoma kwa sababu mara nyingi huwa anapenda kufanya kazi ambazo zinaishi, hivyo alikuwa anatumia muda mwingi sana kutafuta maneno, na kuandika kazi ambazo zinakuwa tofauti na kazi ambazo zinaishi.

"Na kitu kingine kwamba watu wajue ile dili ya Sunday kutoa wimbo mmoja kwa mwaka wasahau tena, napokwambia hapa birthday yangu ni tarehe 14 mwezi huu wa pili siku ya Valentine, nina bonus truck nitatoa, haitakuwa kwa ajili ya Radio wala Tv itakuwa kwa ajili ya mitandao na kwa ajili ya mashabiki wangu na siyo wimbo wa kawaida ni wimbo mkubwa na siku moja utakuja kukaa kwenye TV" alisema Linex Sunday Mjeda.