![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2025/02/18/webbb.jpg?itok=5uNpLPSm×tamp=1739897944)
Pichani Linah Sanga
Akizungumza na mwandishi wetu Linah ameeleza kuwa wimbo huo wa Oletemba umemfanya kukutana na wasanii wakubwa wa nchi tofauti tofauti lakini pia umeweka rekodi ya kuwa msanii wakwanza katika Era yake kufanya kazi nje ya nchi.
Linah pia ameeleza kuwa kwa kipindi kile kilichomkwamisha kuendelea kukimbizana na spidi ya kimataifa ni uongozi uliyokuwa unamsimamia msanii huyo, mbali na hayo pia ameweka wazi kuwa mipango mikubwa ambayo anayo kwasasa ni kuhakikisha anarudi kwenye muziki na huenda akaja na album.