Alhamisi , 12th Feb , 2026

Lil Baby anaripotiwa kutuhumiwa kuhusika katika mzozo na mchezaji wa San Francisco 49ers, Keion White, ambaye muda mfupi baadaye alipigwa risasi.

Pichani ni Lil Baby na Keion White

Siku ya Jumatatu (Februari 9), chombo cha habari cha Bay Area kiitwacho The San Francisco Standard kiliripoti kuhusu tukio hilo la ufyatuaji risasi, lililotokea wakati wa sherehe ya baada ya Super Bowl katika klabu ya usiku ya Dahlia. Shahidi mmoja aliiambia polisi kuwa Lil Baby na kundi lake walijaribu kuingia katika sehemu binafsi ya White, jambo lililosababisha mabishano kati ya Lil Baby na White. Shahidi huyo aliondoka kwenye eneo hilo la klabu kwenda kuwataarifu uongozi, ndipo aliposikia milio miwili ya risasi. Aliporudi, alimkuta White akiwa amepigwa risasi mguuni.

Inaripotiwa kuwa White hakushirikiana na polisi walipomuuliza ni nani aliyempiga risasi. Kwa mujibu wa San Francisco, hakuna mtu aliyekamatwa hadi sasa na polisi hawajamtaja mshukiwa yeyote kuhusiana na tukio hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na timu ya 49ers, White alipata jeraha la risasi kwenye kifundo cha mguu ambalo halikuwa la kuhatarisha maisha, na tayari amefanyiwa upasuaji.

Jarida la XXL limesema limewasiliana na timu ya Lil Baby pamoja na Idara ya Polisi ya San Francisco kwa ajili ya maoni yao kuhusu tukio hilo.