Jumatatu , 9th Oct , 2023

Leo Oktoba 9 imetimia miaka mitano ya kifo cha aliyekuwa Producer wa muziki Tanzania Pancho Latino ambaye alifariki baharini.

Picha ya aliyekuwa Producer wa Muziki Pancho Latino

Producer Pancho Latino amefanya kazi kwenye studio 2 ambazo ni 'Studio 4.12' ya msanii Dully Sykes na 'B Hits' ya Producer Hermy B.

Kazi ya mikono yake ilitubariki mudundo mikali ya muziki kama DSM Stand Up ya Chidi Benz, Bye Bye Joh Makini, Press Play ya DJ Choka, Baadaye sana, Sirudi tena na Dole zote za Mabeste, Nimechokwa na Mdananda za Shetta.