Jumamosi , 6th Feb , 2016

Baada ya kuachia tune kali kabisa ya Kamatia, Aika kutoka Navy Kenzo amesema kutoka kama surprise kwa ngoma hiyo kumeitengenezea nafasi nzuri zaidi, ikiwa kibindoni toka mwezi wa 10 mwaka jana, wakiiachia wakati ambao ngoma Game ikiwa bado ya moto.

Navy Kenzo

Aika amesema kuwa, anaamini kuwa, kuitangaza ngoma hiyo kwa muda wote huo mpaka sasa kungeweza kuwachosha mashabiki, akiamini kuwa Kamatia imewahakikishia nafasi yao kama wasanii wa kimataifa, kutokana na kupokelewa na kukubalika na vituo vyote kitaifa na kimataifa.

Aika amezungumzia pia suala la wao kutajwa kufanya muziki wao katika mahadhi yale yale ya mastaa kama Burna Boy na Patoraking na kuweza kuwateka mashabiki wao kwa kiasi kikubwa, kitu ambacho ameeleza ni dalili na nafasi nzuri kwao kisanaa.