"Kuishi Dar ni darasa tosha" - Cyrill Kamikaze

Jumapili , 12th Sep , 2021

Msanii Cyrill Kamikaze anasema kuishi Jijini Dar es Salaam ni ya darasa tosha kwenye maisha kwa sababu ya matendo,tabia na ujanja ujanja unaofanyika.

Picha ya msanii Cyrill Kamikaze

Cyrill Kamikaze ameshea hilo kupitia page yake ya  Instgram baada ya kupigwa tukio la kuuziwa sabuni akidhani ni simu.

"Kusema ukweli kuishi Dar ni darasa tosha, nilishawahi kuuziwa mche wa sabuni stendi ya Ubungo nikadhani ni simu miaka ya nyuma huko"

"Wale jamaa wa ubungo unaweza ukajua labda ni mateja fulani hivi na wana arosto tu, ila ni watu smart sana akilini. IQ ni kubwa mno unaibiwa kwa technic ya hali ya juu unashindwa kuelewa, na sio kiini macho wala"

"Wanacheza na body language kama vile wana wasiwasi kwaio utoe hela haraka maana simu sijui wameiba dukani huko, sitakuja kuwasahau aise"