Jumatano , 5th Jan , 2022

Kupitia instagram ya msanii Mhe Temba ameshea taarifa za msanii mwenziye KR Mulla Jibaba kwa kuondokewa na baba yake mzazi Mzee Ziada huko mkoani Lindi.

Picha ya KR Mulla

Post hiyo ya Temba inaeleza kuwa "Pole Sana KR Mulla TMK kwa kuondokewa na Baba yako mzazi Mzee Ziada hakika kazi ya Mungu haina makosa. Mzee Ziada amefariki usiku huu huko mkoani Lindi taratibu zote tutawajuza asubuhi kupitia mfiwa na familia, RIP Mzee Ziada".

Mhe Temba, KR Mulla, Dollo na Juma Nature kwa pamoja wanaunda kundi la TMK Wanaume.