Alhamisi , 8th Oct , 2015

Ziara kubwa ya star wa muziki wa Jamaica Konshens katika bara la Afrika inatarajiwa kuanza kwa burudani kali ambayo msanii huyo atafanya nchini Kenya siku ya leo kabla ya kuelekea Juba huko Sudan na baadaye Zimbabwe.

Staa wa muziki wa dancehall kutoka Jamaica Konshens

Burudani ya star huyo itaambatana na wadogo zake Darrio pamoja na Delus ambao nao pia wapo katika jiji la Nairobi nchini Kenya, ujio wa Konshens ukiwa umebarikiwa na mapokezi mazito ya Babyone, msanii kutoka Sudan ambaye anafanya kazi zake kwa sasa nchini Kenya.

Konshens ambaye hii si mara yake ya kwanza kutumbuiza ndani ya Afrika Mashariki, anabaki katika kumbukumbu za watu kwa kuweza kumiliki jukwaa bila madansa wa kike jukwaani kama ilivyozoeleka maonyesho ya wasanii kutoka Jamaica.