Jumatatu , 8th Aug , 2022

Staa wa muziki barani Afrika kutokea nchini Nigeria, Oluwatobiloba Daniel Anidugbe maarufu kama Kizz Daniel amekamatwa na jeshi la polisi nchini siku ya leo, baada ya kushindwa kutumbuiza katika tamasha alilopaswa kutumbuiza usiku wa kuamkia leo.

Kizz Daniel.

Staa huyo anayetamba na wimbo wake wa ''Buga'' alipaswa kutumbuiza siku ya jana katika ukumbi wa Warehouse ambao zamani ulikuwa unatambulika kwa jina la Next Door Arena.

Baada ya kushindwa kutokea ukumbini waandaji wa shughuli hiyo walikwenda polisi kuripoti, na leo amekamatwa na polisi katika hoteli aliyofikia na kufikishwa katika kituo cha polisi cha Oysterbay