Jumatatu , 30th Oct , 2023

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti taarifa ya kuuzwa kwa kitambulisho cha garezani cha marehemu Tupac Shakur pamoja na picha zake zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye kitabu wakati akiwa gerezani.

Picha ya kitambulisho cha Tupac Shakur akiwa gerezani

Kitambulisho chake hicho cha gerezani na picha zake zimepatikana wakati akiwa gereza la Clinton Correctional Facility jijini New York mwaka 1995 na vitapigwa bei ya USD 75,000 sawa na Tsh Milioni 187.

Kibongobongo pia wapo mastaa ambao washawahi kukaa gerezani kama TID, Babalevo, Kajala, Elizabeth Michael 'Lulu' na Jacqline Cliff.

Yupi ambaye unaweza kununua picha yake akiwa gerezani.