Alhamisi , 24th Sep , 2015

Mrembo aliyekuwa anashikilia taji la Miss Uganda, Leah kalanguka na mwanariadha maarufu wa nchi hiyo Stephen Kiprotich wamejipatia nafasi ya kuigiza katika moja ya projekti kubwa ya filamu inayotambulika kwa jina SIPI ambayo inatayarishwa huko nchini

Mrembo aliyekuwa anashikilia taji la Miss Uganda, Leah kalanguka

Filamu hiyo ambayo inangojewa kwa hamu baada ya kutiwa nakshi na uwepo wa mastaa hao, inabeba kisa cha mapambano ambayo wanapitia vijana, katika kujikwamua kimaisha hasa baada ya kukumbwa na majanga ya kiasili, kisa hili kikilenga maporomoko ya Ardhi yaliyotokea huko Budada Uganda.

Waigizaji wengine watakaoshiriki katika filamu hiyo ni pamoja na Nkakalungi Patrick, Blessing Naturinda, Stephen Katusiime, Night Simonela na Abdul Rahim.