Ijumaa , 1st Jan , 2016

Wakili wa mchekeshaji mkongwe Marekani Bill Cosby amesema shitaka la shambulio la ngono linalomkabili mteja wake huyo linamsukumo wa kisiasa.

Mchekeshaji mkongwe wa nchini Marekani Bill Cosby

Akiongea katika kipindi cha runinga wakili Monique Pressley amesema mwendesha mashtaka wa kesi hiyo hataki haki ila anashinikiza kutimiza ahadi za kampeni.

Zaidi ya wanawake 50 wamemtuhumu Cosby kwa kutumia dawa za kulevya pamoja na pombe na kisha kuwadhalilisha kingono. Jumatano wiki hii alifunguliwa shtaka rasmi la kwanza huko Pennsylvania.