Jumapili , 27th Sep , 2015

Rapa Keko wa nchini Uganda, ameweka wazi namna matumizi ya vilevi ikiwepo uvutaji wa bangi vilivyotaka kumpoteza katika ramani, huku rafiki zake wa karibu wakiwa kwa sehemu kubwa ndio waliochangia yeye kujiingiza na kukolea katika tabia hizo.

Rapa Keko wa nchini Uganda

Keko amesema kuwa, vilevi hivyo vilimbadilisha na kuwa mvivu akipoteza msukumo wa kufanya muziki, ambapo baada ya kujifikiria sana kwa msaada wa familia aliweza kutafuta msaada katika kituo cha Serenity kilichopo huko Entebbe Uganda.

Kauli hiyo ya Keko inakuja pia kama ushauri kwa vijana ambao wanajikuta wakipotea katika madawa na kushindwa kuondokana nayo, ambapo binafsi anasimama kama mfano kuwa kubadilika inawezekana.