Akizungumza na eNEWZ Kassim anasema "Ni kweli huwa napata mapokezi makubwa sana Mombasa, na nikifanya show mpaka watu hufikia kutokwa na machozi".
Lakini akaongeza kuwa mapokezi hayo kwa wasanii wa Bongo huyapata sehemu nyingi za nje ya Tanzania wanapokwenda huko kwa shughuli zao mbalimbali za mziki.
Lakii mwisho Kassim alilalamikia jinsi watanzania wanavyowapuuzia wasanii wao akisema "Ujue hapa Bongo kila mtu anajiona staa, anaweza akawa ansikiliza nyimbo yako kwenye simu yake na anakupenda sana lakini bado anapokutana na wewe haoneshi kuthamini ile kazi yako".




