Jux ampongeza Vanessa Mdee

Jumatano , 8th Sep , 2021

Baada ya Vanessa Mdee na mpenzi wake Rotimi kuweka wazi kuwa wanatarajia kupata mtoto siku za hivi karibuni, mpenzi wake wa zamani Jux awapongeza.

Picha ya Pamoja Vanessa Mdee na Rotimi

Kupitia wimbo wake mpya ‘Sina Neno’  King Of Hearts amemtakia kheri na kumuombea maisha mema na yenye furaha baada ya kuiona familia ikikuwa.

Moja ya line kutoka kwenye wimbo huo inasema “Tushafunika kurasa mambo ya zamani yalishapita, maisha mengine sasa kuwa na amani hakuna vita, sikuchukii nakuombea maisha mema na ya furaha, Mungu aonyeshe njia”