Ijumaa , 6th Jun , 2014

Msanii wa muziki Juliani, baada ya kuachia albam yake mpya ya Exponential Potential, ameweka wazi kuwa kumekuwa na changamoto katika swala zima la usambazaji.

Juliani akitumbuiza stejini

Juliani kwa upande wake ameamua kuweka makubaliano na mtandao maarufu nchini Kenya kwa ajili ya kusimamia mauzo ya kazi hii akielezea kwamba njia hii ya pekee itasaidi mashabiki wake kujua ni wapi watapata kazi zake halisi na pia zitawafikia walipo kwa urahisi zaidi.

Kupitia njia hii msanii huyu ametengeneza uhakika wa kudhibiti mauzo ya kazi hii yenye nyimbo 12, ikiwepo ngoma kali ya Morio and Juliet, MH370, Masterpiece, Shuka Roho na nyinginezo.