Alhamisi , 25th Jun , 2015

Mchakato wa mpambano mkali kabisa wa kuwasaka wakali wa kudansi kupitia mashindano ya Dance 100% 2015, umeanza kufuka joto kwa nguvu ya kutosha, ikiwa ni ishara ya maandalizi kufikia hatua za mwisho tayari kabisa kwa kuanza usahili hivi karibuni.

Dance 100

eNewz ikiwa inafuatilia kila hatua kwa karibu kabisa, leo hii tumekutana na T-Bway 360, ambaye anazungumza kwa niaba ya timu kubwa kabisa ya waratibu nyuma yake, akitoa wito kwa vipaji mbali kutoka ndani na nje ya Dar es Salaam kujiweka fiti tayari kwa kuchuana vikali katika Dance100%.

Kuhusiana na tarehe ya kuanza kwa mashindano ya Dance100% 2015, tuendelee kufuatiliana kwa karibu kabisa kupitia EATV na East Africa Radio tuweze kujuzana kila hatua juu ya kile kinachoendelea.