Ijumaa , 7th Jan , 2022

Unaikumbuka Don't Bother ya Joh Makini ft AKA? unaambiwa wimbo huo umezua maneno huko Twitter baada ya Meneja wa Diamond Platnumz Sallam SK kusema ameunganisha ngoma hiyo kufanyika bila malipo yoyote.

Picha ya Sallam SK kushoto, kulia ni Joh Makini

Joh Makini aka-comment kwenye post hiyo kwa kusema Sallam aelezee ameiunganisha vipi kwani alipambana sana kukwamisha wimbo huo usifanyike. 

"Aelezee aliunganisha vipi yeye sio chanzo cha hiyo collabo, kwa mazingira niliyofanya collabo na AKA nitawashukuru sana Nikki wa Pili na G NakoWarawara lakini waliomleta walikua hawataki itokee".

"Muarabu alipambana sana kukwamisha hii basi tu Mwenyezi Mungu hajawahi kushindwa" ameandika Joh Makini