Kuhusu kushindanishwa, kufananishwa na kuletewa tofauti na baadhi ya wasanii wa HipHop Bongo, Joh Makini, ameeleza kuwa hali hiyo haijamuathiri kitu chochote na hakuja kwenye muziki ili kushindana na mtu.
"Mimi nachukulia vitu vya kawaida kwenye kitu chochote chenye ushindani, watu wamekuwa na mawazo tofauti tofauti, nilichokuwa nafanya ni kuzingatia kwa kile ninachoamini, sijawahi kuamini kama kutengenezewa tofauti yeyote inaweza kuniongezea kitu chochote, kwenye Game yangu huwa nachukulia kawaida tu kwa sababu mimi hainiathiri chochote na sikuja kwenye game kushindana na mtu yeyote" amesema Joh Makini.
Aidha akizungumzia kuhusu uwepo wa mitandao ya kijamii ambayo inachukua nafasi kubwa sana kwenye maisha ya watu sasa hivi Joh Makini, amesema anachukulia hivo kama ni mabadaliko ya kidunia ambayo huwezi kuyazuia.
Akiongelea madhara ya mitandao ya kijamii kama kudhalilishana, kushambuliwa na kutukanwa Joh Makini amesema.
" Watu kushambuliwa na kutukanwa hiyo ipo tangu dunia ilipoanza hata Yesu alishambuliwa alitukanwan hadi wakamsulubisha kwenye msalaba na sio kitu kigeni kwenye dunia"