
msanii wa muziki wa Marekani Joe Thomas
Joe Thomas katika safari hii, ametua nchini humo na mtoto wake wa kike na atafanya onyesho sambamba na mpiga gitaa mwenye rekodi ya kushinda tuzo za Grammy, Norman Brown.
Ujio wa msanii huyu unawapatia wapenda burudani Afrika Mashariki hususan huko Uganda nafasi nyingine ya kuburudika kutoka kwa msanii huyu, ikiwa ni miaka 7 imepita tangu onyesho lake la mwisho nchini humo.
