Jumatatu , 28th Apr , 2014

Msanii mahiri wa maigizo hapa nchini Tanzania, Jacob Steven maarufu zaidi kama JB, ameweka wazi kuwa mafanikio yake makubwa katika sanaa hiyo kwa sasa, mwanzo wake kabisa ilikuwa ni ushawishi kutoka kwa msanii mwezake, Single Mtambalike aka Richie.

JB ameweka wazi kuwa, katika hatua zake za awali kuingia katika uigizaji, alikuwa akipata msukumo kutoka kwa Richie na kwa sehemu, alikua akifanya sanaa hii ili kumridhisha rafiki yake huyu, na si kwa ajili ya malengo ya kuja kuwa mwigizaji mkubwa.

Msanii huyu amesema kuwa, baada ya jitihada hizi za awali za Richie kumvuta katika sanaa ya maigizo, kwa sasa kazi hii imekwishakuwa sehemu ya maisha yake huku akiwa na kazi bora kabisa sokoni, akiwa mmiliki wa kampuni ya utayarishaji filamu ambayo ameipatia jina Jerusalema.