Jumatatu , 14th Nov , 2016

Msanii wa taarabu nchini Khadija Yusuph amesema hakuna tena kundi la Jahazi Morden Taarabu kwa sasa na tayari wamegawana vitu vilivyokuwa ndani ya kundi hilo na yeye kwa sasa yupo kwa Thabit Abdul.

Khadija Yusuph

 

Akiongea ndani ya eNews Khadija amesema Jahazi limevunjwa na Mwenyezi Mungu kwa kuwa Mzee Yusuph wakati anaacha muziki alisema hata vunja kundi hilo lakini Mungu mwenyewe ndo atalivyunja na tayari dua yake imepokelewa na Mungu.

Pia Khadija amesema kwa sasa furaha ya kaka yake Mzee Yusuph imekamilika kwa sasa na dua zake pia zitakuwa  zimepokelewa na Mungu kama alivyokuwa akiomba kwamba ifikie kipindi hata nyimbo zake zisiwe zinapigwa.