Jumamosi , 6th Jun , 2015

Msanii Jaffarhymes ambaye usiku wa jana ametambulisha ujio wake mpya katika show ya FNL kupitia v

Jaffarhymes

Msanii Jaffarhymes ambaye usiku wa jana ametambulisha ujio wake mpya katika show ya FNL kupitia video ya ngoma yake mpya ya Wakati, amekiri kuwa ni vigumu sana kwa msanii ambaye amekaa kimya kwa muda mrefu, kuweza kurejea na kutikisa chati kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma.

Star huyu ambaye anaonesha kuwa amejipanga vilivyo na amepania kazi yake, ameithibitishia eNewz kuwa amelisoma soko vizuri na kuzikamata mbinu zote za kurudi katika kiki yake, na haya ni baadhi ya mambo ambayo mkali huyu baada ya utafiti wake ameyagundua, akiwa kihesabu zaidi akizingatia tempo - kasi ya mdundo wa muziki kufikia 180 ambazo ndiyo inahusika katika ngoma nyingi kwa sasa.

Jaffaray amesema kuwa, kwa mapokezi ambayo ameyapata, licha ya kuacha jina kubwa katika game amegundua ni kazi ngumu kufukia alipofikia sasa baada ya kimya cha muda, akieleza kuwa amefarijika kuona kazi yake inafanya vizuri katika chati mbalimbali, akikiri kuwa kwa mabadiliko ya sasa inahitaji nguvu ya ziada kuisukuma ngoma ili izidi kufanya vizuri.